Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahisani wa kimataifa wahaidi kutoa euro milioni 300 kuwasaida waathirika wa vita vya Balkans

Wahisani wa kimataifa wahaidi kutoa euro milioni 300 kuwasaida waathirika wa vita vya Balkans

Wahisani wa kimataifa wamehaidi kiasi cha euro milioni 300 kwa ajili ya kuwasaidia mamia ya wakimbizi waliokosa makazi kufutia machafuko yaliyozuka katika miaka ya 90 katika eneo la Balkans.

Kiasi hicho cha fedha kinatazamiwa kutumika kuwaandalia makazi ya kuishi zaidi ya watu 74,000 ambao walikwenda uhamishoni baada ya kuzuka kwa machafuko hayo.

Ujenzi wa nyumba mpya unatazamiwa kukamilika katika kipindi cha kati ya miaka mitatu mpaka mitano ijayo na hivyo kuwafanya wakimbizi pamoja na wale raia wa ndani walikosa makazi kupata hifadhi.

Wakati wa machafuko hayo, zaidi ya watu 200,000 walipoteza maisha na wengine wapatao milioni 2 walikosa makazi.