Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM, Thailand na Canada kujenga uwezo wa kukabili usafirishaji haramu wa binadamu

IOM, Thailand na Canada kujenga uwezo wa kukabili usafirishaji haramu wa binadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, kwa kushirikiana na serikali kadhaa ikiwemo Thai, na Canada wiki hii litazindua mpango maalumu wenye shabaha ya kuijengea uwezo mamlaka ya Thailand jinsi ya kukabiliana na tatizo la usafirishaji watu kwa magendo.

Katika utekelezaji wa mpango huo, IOM inatazamiwa kusaidiana na jeshi la polisi la nchi hiyo pamoja na ubalozi wa Candan nchini Thailand.

Lengo kuu na kujaribu kudhibiti jaribio lolote la usafirishaji haramu wa watu unaofanywa kwenye eneo hilo, iwe kuingia nchini humo ama kutoka nchini humo na kwenda kwingine.

Mpango huo ambao utatekelezwa katika maeneo ya mipakani unafadhiliwa na serikali ya Canada, ambayo imechukua hatua hiyo kufuatia ziara aliyoifanya hivi karibuni Waziri Mkuu wa Stephen Harper.