Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaanzisha programu ya kukutanisha familia kati ya Sahara Magharibi na Tindouf

UNHCR yaanzisha programu ya kukutanisha familia kati ya Sahara Magharibi na Tindouf

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanzisha safari yake ya kwanza ya ndege kwenye programu za kukutanisha familia zilizotengwa kwa muda mrefu za Sahrawi kwenye kambi za Tindouf nchini Algeria na eneo la Sahara Magharibi.

Ndege aina ya Boeng 737 iliwasafirisha watu 150 wa familia hizo kutoka eneo la Sahara Magharibi kwenda kwa kambi nchini Algeria na kurejea na wakimbizi 137 wa Sahrawi kutoka kambi za Tindouf na kuwapeleka eneo la Sahara Magharibi. Wengi wa wakimbizi wa Sahrawi wamekuwa wakiishi jangwani kwa zaidi ya miaka 35. Hata hivyo wengine waliishi kwenye eneo la Sahara Magharibi na hadi sasa jamaa hizo zimesalia kutenganishwa.