Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chama cha posta cha UM chamiliki muhuri wa kwanza duniani

Chama cha posta cha UM chamiliki muhuri wa kwanza duniani

Chama cha Posta cha Umoja wa Mataifa kimetangaza kuwa kwa sasa kinamiliki kile kilichotaja kama muhuri maarufu zaidi duniani uliotolewa miaka 172 iliyopita na ulio na picha ya Victoria, ambaye ni malkia wa zamani wa uingereza. Kando na muhuri huo pia chama hicho kwa sasa kinamiliki mihuri mingine miwili iliyo na picha za Victoria na pia bahasha iliyo na nembo ya mhuri huo.

Muhuri huo utaongezea idadi ya mihuri inayomilikiwa na chama cha posta cha Umoja wa Mataifa ambayo kwa sasa ni mihuri 800,000. Mihuri hiyo ina gharama ya Franca 1965 pesa za Uswisi.