Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Afisa wa Serbia kujadilia mkwamo wa Kosovo

Ban akutana na Afisa wa Serbia kujadilia mkwamo wa Kosovo

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-moon amekuwa na mazunguzmo na waziri wa mambo ya Nje wa Serbia Vuk Jeremic na kujadilia masuala kadhaa hasa hatua zilizopigwa juu ya utanzuaji wa mzozo wa Kaskazini mwa Kosovo.

Viongozi hao wamepongeza maendeleo mema yanayoendelea kujiri wakati huu ambapo Umoja wa Ulaya ukiwa kwenye mstari wa mbele kusaka usuluhisho baina ya pande zinazozana Pristina na Belgrade.

Ban amepongeza nafasi iliyochukuliwa na Belgrade iliyoonyesha utayari wake kupunguza hali ya wasiwasi kwenye eneo hilo jambo linaloashiria kupatikana kwa amani ya kudumu.

Ama Ban amemtaka waziri huyo wa mambo ya nje kuongeza mashirikiano kwa vikosi vya kimataifa vya ulinzi wa amani kwenye eneo hilo ili kukamilisha mapema shabaha ya kupatikana kwa amani.