Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za kiarabu zina fursa sasa ya kujenga mustakhbali zinaostahili kuwa nao:Ban

Nchi za kiarabu zina fursa sasa ya kujenga mustakhbali zinaostahili kuwa nao:Ban

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anayezuru Jordan hivi sasa ameuambia mkutano na waandishi wa habari uliojumuisha pia waziri wa mambo ya nje wa Jordan Nasser Judeh mjini Aman kwamba eneo la nchi za Kiarabu zina fursa kubwa ya kuwa na mustakhbali waliokuwa wanautaka.

Ban ambaye amejadili pia changamoto zinazolikumba eneo hilo amesema katika wakati huu amejizatiti kuunga mkono mabadiliko yanayoendelea katika ulimwengu wa Kiarabu, juhudi za watu kuhakikisha wanapata demokrasia, haki za binadamu na fursa za kiuchumi.

Ban ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo lazima wanawake na vijana wawezeshwe. Pia viongozi hao wawili wamejadili hali ya Syria ambapo Ban amesema ni muhimu sana hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote kumaliza machafuko Syria.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)