Mjumbe wa UM kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar kulizuru taifa hilo

30 Januari 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana atafanya ziara nchini Myanmar kati ya Januari 31 na Februari mwaka huu kwa mwaliko wa serikali.

Ojea Quintana anasema kuwa wanashuhudia maendeleo nchini Myanmar na ziara hii inajiri wakati kunapoandikwa historia kubwa nchini humo. Wakati wa ziara hiyo ya siku sita mtaalamu hiyo aliyetwikwa jukumu na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza hali nchini Myanmar atakutana na mawaziri wa serikali , wabunge, tume ya haki za binadamu iliyobuniwa hivi majuzi na washika dau wengine.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter