Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM kuhusu haki ya nyumba kuizuru Israel na Palestina

Mjumbe wa UM kuhusu haki ya nyumba kuizuru Israel na Palestina

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye haki ya kuwa na nyumba Raquel Rolnik ataitembelea Israel na eneo la kipalestina linalokaliwa na Israel kwenye ziara ambayo itango’a nanga n tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 12 mwezi Februari. Ziara hiyo itaaangazia masuala kadhaa yakiwemo upatikanaji wa nyumba, hali ya makundi yaliyotengwa na suala la kuwahamisha watu kwa lazima.

Wakati wa ziara yake mjumbe huyo atakutana na wawakilishi kutoka kwa serikali ya Israel na kutoka kwa utawala wa Palestina na pia kutoka kwa mashirika ya kimataifa na ya umma.