Uchunguzi waanzishwa baada ya madawa ya Coccaine kupatikana kwenye UM

Uchunguzi waanzishwa baada ya madawa ya Coccaine kupatikana kwenye UM

Uchunguzi umeanzishwa baada ya mfuko uliokuwa na kilo 16 za madawa ya kulevya ya Coccaine kupatikana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Madawa hayo yaligunduliwa juma moja lililopita kwenye mfuko huo ulio na nembo bandia ya Umoja wa Mataifa. Mfuko huo kwa sasa umekabidhiwa utawala wa Marekani. Katibu wa masuala ya ulinzi na usalama kwenye Umoja wa Mataifa Gregory Starr anasema kuwa hiyo ni kazi ya walanguzi wa madawa ya kulevya.

(SAUTI YA GREGORY STARR)