Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sherehe za kuwakumbuka waliouawa kwenye mauaji ya Holocaust zaandaliwa

Sherehe za kuwakumbuka waliouawa kwenye mauaji ya Holocaust zaandaliwa

Maafisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa wametaka kulindwa watoto kutokana na athari za kivita. Afisa huyo ameyasema hayo wakati wa shughuli ya kuwakumbuka karibu wayahudi milioni 6 waliouawa na utawala wa wa kinazi wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. K

atibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwa upande wake amesema kuwa watoto milioni moja waliangamia wakiwemo watu walemavu. Ban amesema kuwa wengi walikufa kutokana na njaa na magonjwa na wengi kubaki mayatima akiongeza kuwa haitabainika kile ambacho wote hao wangechangia kwa dunia kama wangeishi.