Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya kukiunganisha kisiwa cha Cyprus kung’oa nanga

Mazungumzo ya kukiunganisha kisiwa cha Cyprus kung’oa nanga

Mazungumzo ya kukiunganisha kisiwa cha Cyprus yanatarajiwa kung’oa nanga Jumapili hii kukiwa na matumaini kwamba huenda kukaafikiwa makubaliano kati ya jamii hizo mbili hasimu. Uhasama kati ya jamii ya Cypriot nchini Ugiriki na ile ya Cypriot nchini Uturuki ulianza kwenye kisiwa hicho cha bahari ya Mediterranean mwaka 1974 ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukijaribu kutafuta suluhu kwa miongo kadha sasa.

Michel Bonnardeaux, ambaye ni msemaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Cyprus UNFICYP anasema kuwa kuna matumaini kuwa mpango huo wa kuleta mapatano uataendelea mbele.

(SAUTI YA MICHEL BONNRDEAUX)