Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ni muhimu katika kuzuia mizozo:Baraza la Usalama la UM

Sheria ni muhimu katika kuzuia mizozo:Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepinga vikali kutolewa msamaha kwa wale wanaopatikana kuendeleza ukiukwaji wa haki za binadamu. Pia baraza hilo limesisitiza umuhimu wa kuheshimiwa kwa sheria kama moja ya njia ya kuzuia mizozo, kwa utatuzi wa mizozo na katika uwekaji amani.

Baraza hilo pia limetangaza kujitolea kwake katika kuhakikisha kutekelezwa kwa sheria ya kimataifa. Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi huu ni Maite Nkhoana Mashabane kutoka Afrika Kusini.