Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyota wa Kriketi Pakistani kuhubiri madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya

Nyota wa Kriketi Pakistani kuhubiri madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya

Nyota wa mchezo wa kriketi raia wa Pakistan Shahdi Afrid anatazamia kutokezea hadharani kuzungumzia madhara mabaya juu ya matumizi ya madawa ya kulevya. Akiwa mjumbe wa hisani wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha na utokomezaji wa madawa ya kulevya na vitendo vya uhalifu UNODC, nyota huyo anataka kutuma ujumbe juu muhimu wa michezo katika uimarishaji wa afya.

Afridi, amepata kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Pakistan kuanzia mwaka 2009 hadi 2011. Alipamba duru za kimataifa mnamo mwaka 1996 pale akiwa bado kijana mdogo kabisa wa umri wa miaka 16 alipofanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa kwa kupata ushindi wa kishindo.

Mwanamichezo huyo anasema kuwa anapinga na kuchukia vilivyo matumizi ya madawa ya kulevya, hivyo ameamua kusimama hadharani kuelezea madhara yatokanayo na matumizi ya madawa hayo.