Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa kulinda amani wapelekwa kuzuia mashambulizi ya kulipiza kisasi Sudan Kusini

Wanajeshi wa kulinda amani wapelekwa kuzuia mashambulizi ya kulipiza kisasi Sudan Kusini

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamepelekwa ili kuzuia mashambulizi ya kulipiza kisasi kwenye jimbo la Jongley Sudan Kusini.

Hivi karibuni takriban vijana 7000 wenye silaha kutoka kundi la kikabila la Lou Nuer waliwashambuliwa wapinzani wao wa jamii ya Murle kwenye miji ya Likuanole na Pibor la kulazimisha maelfu ya watu kukimbia.

Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini Hilde Johnson anasema watu wameanza kurejea taratibu kwenye miji waliyokimbia lakini hali ya kibinadamu bado ni mbaya.

(SAUTI YA HILDE JOHNSON)