Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amelaani vikali shambulio la kigaidi nchini Pakistan

Ban amelaani vikali shambulio la kigaidi nchini Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la leo la kigaidi kwenye mji wa Jamrud Kaskazini Magharibi mwa Pakistan. Shambulio hilo limekatili maisha ya watu na kujeruhi wengine wengi wakiwemo watoto.

Ban ametuma salamu za rambirambi na pole kwa familia za waathirika na kurejea wito wake wa mshikamano wa Umoja wa Mataifa kwa watu na serikali ya Pakistan katika juhudi zao za kuendelea kukabiliana na ugaidi na itikadi kali.