Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shule ya sheria Croatia yapata msaada wa vitabu kutoka mahakama ya ICTY

Shule ya sheria Croatia yapata msaada wa vitabu kutoka mahakama ya ICTY

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Yugoslavia ya zamani ICTY imetoa msaada wa vitabu na nyaraka kwa shule ya masuala ya sheria ya chuo kikuu cha Zagreb Croatia.

Mahaka ya Umoja wa Mataifa ya ICTY inawahukumu watu wanaoshutumiwa kutekeleza makosa makubwa ya ukiukaji wa sheria za kimataifa katika Yugoslavia ya zamani wakati wa vita ambavyo vilishuhudia nchi hiyo ikigawika mapande mwanzoni mwa miaka ya 1990. Mahakama hiyo ambayo karib inakamilisha muda wake inasema msaada huo ni jukumu lake la kuchagiza kuheshimiwa kwa utawala wa sheria katika kanda hiyo.