Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la afya ya uzazi nchini Burundi

Suala la afya ya uzazi nchini Burundi

Makala yetu ya wiki hii inaangazia hatua zilizopigwa nchini Burundi kuhusu suala la afya ya uzazi hasa katika kupunguza vifo vya akina mama wakati wanapojifungua.

Takwimu za Mradi wa kitaifa wa afya ya uzazi zinaonyesha kwamba Burundi inaweza kuwa tayari kutekeleza lengo hilo la tano la Milenia kabla ya mwaka wa 2015. Mafaniko hayo yamepatikana kutokana na hatua za kujifungua bora kwa kina mama waja wazito.

Hata hivo changamoto kubwa bado ni ongezeko kubwa la idadi ya watu. Serikali ya Burundi imeanza kuchagiza kuweka mbioni mpango wa kukadiria idadi ya watoto kwa kila familia kwa kuzingatia huduma za mipango ya uzazi.