Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliokimbia ghasia kwenye mji wa Pibor Sudan Kusini warejea makwao

Waliokimbia ghasia kwenye mji wa Pibor Sudan Kusini warejea makwao

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS unasema kuwa watu waliokimbia ghasia za kikabila kwenye mji wa Pibor ulio kwenye jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini kwa sasa wanarejea makwao. Mapema juma hili wanajeshi wa Sudan kusini wa Sudan People’s Liberation Army SPLA waliwafyatulia risasi vijana waliojihami kutoka kabila la Lou Nuer waliouvamia mji huo.

Kuliripotiwa karibu vijana 6000 waliouzingira mji wa Pibor ambao ni nyumbani kwa jamii ya Lou Nuer. Msemaji wa UNMISS Kouider Zerrouk anasema kuwa hali kwenye mji wa Pibor sasa ni tulivu.

(SAUTI YA KOUIDER ZERROUK)