Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wasiokuwa na jira kwenye ukanda wa Gaza bado ni juu

Idadi ya wasiokuwa na jira kwenye ukanda wa Gaza bado ni juu

Ripoti kutokosa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi wa kipalestika kwenye ukanda wa Gaza inasema kuwa idadi ya wakimbizi wasiokuwa na ajira kwenye eneo hilo ni ya asilimia 33.8 ishara idadi kubwa ya wakimbizi hawafanyi kazi hata baada ya kuongezeka kwa nafasi za ajira kwenye sekta ya ujenzi.

Ripoti hiyo inaelezea kwamba wakimbizi 1,430 zaidi waliajiriwa kwenye Sekta ya umma huku 18,670 wakiajiriwa kwenye sekta za kibinafsi. Ripoti hiyo pia iligundua kuwa kuliongeza nafasi za ajira kwenye sekta ya kibinafsi kutokana na kuingizwa kwa bidhaa za ujenzi katika eneo hilo.