Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti yapiga hatua miaka miwili baada ya tetemeko la ardhi

Haiti yapiga hatua miaka miwili baada ya tetemeko la ardhi

Karibu miaka miwili baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 taifa hilo linaonyesha dalili za kusimama tena. Hii ni kulingana na afisa wa Umoja wa Mataifa ambaye anasema kwamba jitihada za ujenzi mpya zinapaswa kupewa kipaumbele.

Akihutubia waandishi wa habari mjini New York naibu mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti Nigel Fisher anasema kwamba hatua zimepigwa kwenye sekta ya elimu, afya , ajira na miundo.