Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea kusikitishwa kwake kufuatia kuuwa kwa askari wa Uturuki na vikosi vya Kurdistan

Ban aelezea kusikitishwa kwake kufuatia kuuwa kwa askari wa Uturuki na vikosi vya Kurdistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea shaka  juu ya taarifa za kuwepo machafuko yaliyoshuhudia askari 26 wa Uturuki wakipoteza maisha baada ya kuvamiwa na vikosi vya Kikurd katika eneo la KusinI mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa mashambulizi hayo yalifanyika katika jimbo la Hakkari na askari wa Kurdistan wakiendesha hujuma hiyo kutokea nchini Iraq. Akielezea masikitiko yake, Ban amesema kuwa kitendo hicho hakikubaliki hasa inapojitokezea mpaka wa taifa moja kutumika kutimiza vitendo vya mauaji.