Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yatakiwa kuruhusu wataalamu wa haki za binadamu kuingia nchini humo

Syria yatakiwa kuruhusu wataalamu wa haki za binadamu kuingia nchini humo

Utawala wa Syria umetakiwa kuwaruhusu wataalamu huru wa kimataifa wa haki za kibinadamu kuzuru nchi hiyo ili kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu ambao umefanyika nchini humo tangu kuanza kwa ghasia mwezi Machi.

Hii ni kwa mujibu wa Paulo Sergio Pinheiro mkuu wa tume ya wanachama watatu iliyoteuliwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ya kuendesha uchunguzi huo. Pinheiro anasema kuwa wanataka kuanza uchunguzi huo haraka iwezekanavyo.

“Ninajaribu kusisitiza kuwa sio kwa manufaa yetu bali pia kwa manufaa ya serikali ya Syria. Natumai itakuwa rahisi sisi kukuta na ujumbe ambao unakuja kwenye warsha ya UPR Ijumaa ijayo.”

Mwezi Agosti ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisafiri kwenda Syria kukadiria mahitaji ya kibinadamu yaliyosababishwa a ghasia za kisiasa zinazoendelea nchini humo.