Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kuwe na uwajibikaji kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka

Ban ataka kuwe na uwajibikaji kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kim-moon ametaka kuwepo njia iliyo wasi kwenye uchunguzi wa vitendo vilivyotekelezwa wakati wa kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka. Ban ametaka kutumika kwa mpango aliuoutia sahihi na rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa Mei mwaka 2009 baada ya kumalizika vita kati ya serikali na wanamgambo wa Liberation Tigers of Tamil Eelam (LTTE).

Mapema mwezi huu Ban aliwasilisha ripoti ya jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uwajibikaji wakati wa vita hivyo mbele ya baraza la haki za binadamu na ofisi ya kamishina wa haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.