Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasikitishwa na namna machafuko ya Darfur yanavyokwamisha juhudi za upelekaji misaada ya kiutu

UM wasikitishwa na namna machafuko ya Darfur yanavyokwamisha juhudi za upelekaji misaada ya kiutu

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utoaji misaada ya kiutu amezitolea mwito mamlaka katika eneo lililozongwa zongwa na machafuko Darfur kuhakikisha kwamba zinaweka kando tofauti zao ili kufanikisha zoezi la upelekaji wa misaada ya kibinadamu.

Valerie Amos amesema kuwa kumekuwa na mkwamo wa upelekaji wa misaada ya kiutu katika Mji wa Jabel Marra uliopo eneo la Mashariki kutokana na marafuku iliyowekwa na makundi hasimu.

Ametaka mabigwa hao wa mapigano kuepusha tofauti zao za kiitikadi na kisiasa ili kuruhusu upekekaji wa misaada kwenye eneo hilo, ambalo limeathiriwa na mapigano yaliyozuka upya.

Ama kukosekana kwa usalama na machafuko ya mara kwa mara katika jimbo la Darfur kumekwamisha juhudi za mashirika ya utoaji misaada kuwafikia mamia ya watu kwenye eneo hilo.

Wafanyakazi wa kimataifa ambao wanahusika na utoaji misaada wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana usalama, na baadhi yao wamekuwa wakiangukia mikononi mwa wahalifu.

Tangu march mwaka jana 2009