Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la AU lafanikiwa kudhibiti Moghadishu kutoka kwa Al-shabaab

Jeshi la AU lafanikiwa kudhibiti Moghadishu kutoka kwa Al-shabaab

Jeshi la kulinda amani la muungano wa afrika AU nchini Somalia limechukua udhibiti wa mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu baada ya kuwashinda wanamgambo wa al shabab kwenye makabiliano makali.

Kwa muda wa karibu siku kumi wanamgambo wa al shabab walikishambulia kikosi cha muungano wa afrika (AMISON) kenye maeneo yaliyo kando kando mwa bahari mjini Mogadishu.

Ripoti zinasema kuwa wanamgambo wakiwemo pia wapiganaji wa kigeni walisonga mbele na kukaribia majerngo ya bunge na ikulu ya rais hali iliyofanya wanajeshi kutoka Uganda kufanya juhudi na kutumia silaha nzito kuwashinda.

Kamanda wa kikosi cha Uganda nchini Somali Mickael Ondoga anasema mapigano hayo yalishuhudiwa kuanzia tarehe 24 mwezi uliopita baada ya vikosi vya serikali ya mpito ya Somali kuondoka kutoka vituo vyao. Mapigano hayo yalijri baada ya wanamgambo wa al shabab kutangaza oparesheni mpya ya kuwatimua wale iliowataja kama wakristo waliovamia nchi yao.