Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la WHO latangaza kudhibitiwa kwa ugonjwa wa cholera nchini Afghanistan

Shirika la WHO latangaza kudhibitiwa kwa ugonjwa wa cholera nchini Afghanistan

Ugonjwa wa Cholera ambao awali uliripotiwa kuwaathiri karibu watu 130 kwenye wilaya ya Nowa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan kwa sasa umedhibitiwa .

Maradhi hayo yaliripotiwa kwanza tarehe tisa mwezi huu baada ya shirika moja kuripoti visa 60 vya ugonjwa usiojulikana ambao baadaye ulibainika kuwa ugonjwa wa Cholera kupitia utafiti wa mahabara.

Wizara ya afya nchini Afghanistan kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO walianzisha mara moja harakati za kukabiliana na uogonjwa huo huku WHO ikitoa misaada ya madawa. Hadi sasa visa vya waliombukizwa maradhi hayo vinaripotiwa kupungua hadi visa vitatu kwa siku wakati juhudi za kuukabili ugonjwa huo zikiendelea.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Peter Graaff hata hivyo anasema kuwa baadhi ya changamoto zinazokumba shughuli ya kukabiliana na maradhi hayo ni pamoja na suala la ukosefu wa usalama katika seheme kadha za nchi.