Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya watu ni moja ya biashara kubwa haramu Ulaya:UM

Biashara ya watu ni moja ya biashara kubwa haramu Ulaya:UM

Biashara ya watu ni moja ya biashara kubwa haramu barani Ulaya kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo.

Ripoti hiyo imezinduliwa katika hafla maalumu ambapo Hispania imekuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kujiunga na kampeni ya Umoja wa Mataifa dhidi ya usafirishaji haramu wa watu iitwayo Blue Heart Campaign. Ripoti hiyo "Usafirishaji wa watu Ulaya kwa dhuluma ya ngono" iliyotolewa na ofosi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC, inaonyesha kwamba magenge ya wahalifu wanajipatia kiasi cha dola bilioni tatu kwa mwaka kwa kuwanyonya watu kupitia biashara ya ngono na kazi za shuruti ikiwa ni watu 140,000 ambao ni wengi kwa wakati kama huo.

Waathirika wengi mara nyingi huwa ni wasichana wadogo ambao hubakwa, hutendewa ukatili, kufungwa , hupewa mihadarati na mifumo minginye ya unyanyasaji. Duniani kote takribani watu milioni 2.4 ,ambako hadi asilimia 80 ni wanawake na wasichana hivi sasa wananyonywa na kutumiwa kama kama wahanga wa usafirishaji haramu wa watu kwa ajili ya ngono au kutumikishwa kazi ,umesema Umoja wa Mataifa.

Lengo la kampeni hiyo ni kuelimisha kuhusu biashara haramu ya watu , serikali, jumuiya za kijamii, vyombo vya habari na umma kwa ujumla. Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa UNODC Antonio Maria Costa amezitaka nchi zote za Ulaya kujiunga na Blue Heart kampeni.