Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MMKM anadai wapiganaji Usomali wameazimu kupindua serikali halali

MMKM anadai wapiganaji Usomali wameazimu kupindua serikali halali

Mjumbe Maalumu wa KM (MMKM) kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah kwenye taarifa kwa waandishi habari iliotolewa Ijumatano, kutokea Nairobi, aliwashtumu wale watu walioanzisha mashambulio ya kwenye mji wa Mogadishu majuzi, wapiganaji ambao walituhumiwa kuwa na dhamira ya kuiangusha serikali halali ya Usomali, kwa kutumia mabavu na fujo.