Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango ziada wa kimataifa unahitajika dhidi ya maharamia, asema Mjumbe wa KM kwa Usomali

Mchango ziada wa kimataifa unahitajika dhidi ya maharamia, asema Mjumbe wa KM kwa Usomali

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdalla aliwasilisha taarifa maalumu kwa waandishi habari, kufuatia tukio la majuzi kuhusu mapambano na maharamia, nje ya mwambao wa Usomali. Alisema kwenye taarifa kwamba Mataifa Wanachama katika UM yanawajibika kukuza mchango wao katika kukabiliana na kile alichokiita "msiba mkuu wa kimataifa", msiba ambao alidai "husababisha uharibifu mkubwa wa amani ulimwenguni."

Alisisitiza kwamba "ingelikuwa vyombo vya jeshi la majini vya kimataifa vimekosekana kwenye mwambao wa Usomali, vitendo vya uharamia vingfelifurutu ada". Anaamini manowari za kimataifa "ndizo zilizofanya kazi nzuri zaidi ya kulinda shehena za misaada ya chakula [zisinyakuliwe na maharamia]." Kadhalika, Ould-Abdallah alisisitiza "operesheni za karibuni za vyombo vya kijeshi vya Serikali za Marekani na Ufaransa", kukabiliana uso kwa uso na maharmia ni vitendo vilivyowathibitishia wafanyao uharamia, kijumla, pamoja na wale wanaowaunga mkono kwamba hawatoruhusiwa tena, abadan, fursa ya kukwepa adhabu kwa vitendo vyao. Alikumbusha ya kuwa utumiaji wa "kisingizizo cha ufukara na hali ya kukosa matumaini kimaisha, kuwahamasiha vijana wa Usomali kuendeleza uharamia" na wale wanaoongoza vitendo hivyo ni hali isiolingana na madili ya kimataifa.