Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU lapitisha kwa kura nyingi azimio la kusimamisha mapigano Ghaza

BU lapitisha kwa kura nyingi azimio la kusimamisha mapigano Ghaza

Baada ya mivutano na majadiliano ya karibu siku nzima mnamo siku ya Alkhamisi, kwenye Makao Makuu, wajumbe wa Baraza la Usalama, mnamo saa tatu za usiku, walipiga kura ya kupitisha azimio nambari 1860 (2009), liliodhaminiwa na Uingereza, ambalo lilitia mkazo “dharura ya kusimamisha haraka mapigano kwenye eneo la Tarafa ya Ghaza” na kuhakikisha “vikosi vya Israel vitaondoshwa kwa ukamilifu" kutoka sehemu hiyo ya uhasama, na kupendekeza huduma za ugawaji wa chakula, nishati na vifaa vya matibabu kuendelezwa bila pingamizi, pamoja na kadhia nyengine kadhaa za kihali, na kutaka juhudi za kimataifa ziongezwe ili kuzuia kufanya magendo ya silaha.

Baada ya utiaji kura wa azimio, KM alihutubia Baraza la Usalama na alisema umma wa kimataifa umesubiri muda mrefu kwa mapigano kukomeshwa katika Ghaza:

“Katika wiki mbili zilizopita, umma wa kimataifa umeshuhudia

kwa huzuni kuu na kihoro, muongezeko wa vurugu na mateso katika Tarafa ya Ghaza na eneo la Israel kusini, na wameitaka UM kukomesha mapigano. Nimeingiwa moyo na kufarijika na hatua iliochukuliwa na Baraza la Usalama leo hii kupitisha azimio la kukomesha hali hii ya msiba.”

Mataifa 14 yalipiga kura ya upendeleo wa azimio, na nchi moja pekee, Marekani, haikupiga kura upande wo wote.

Nikiripoti kutoka Makao Makuu mjini New York ni AZR kutoka studio za Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM