Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Baraza la Usalama limepitisha Azimio la Raisi wa Baraza lilioshtumu Djibouti kwa vitendo vya kijeshi dhidi ya Djibouti, na kutoa mwito kwa mataifa yote mawili kusiitisha haraka uhasama, na kuitaka Eritrea kuonyesha ustahamilivu na kuharakisha kuondosha vikosi vyake kutoka eneo husika.

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limelaani mauaji ya Hassan Abdi, mmoja wa madereva wa malori yalioajiriwa na UM kugawa tani za metriki 328 za chakula kwenye majimbo ya Bay na Bakool kutokea Mogadishu. Marehemu Abdi aliuawa alfajiori ya Alkhamisi karibu na kijiji cha Leego.

Bodi la Utendaji la WFP limeidhinisha mradi wa miaka minne ulioandaliwa kukabiliana vizuri zaidi na tatizo la kukithiri kwa njaa, kutokana na mifumko ya bei za chakula kwenye soko za kimataifa.

Ujumbe wa KM Ban Ki-moon uliorikodiwa kwenye vidio, na kutangazwa Ijumaa, kuhusu taadhima za Siku ya Amani ya Kimataifa, itakayoadhimishwa miezi mitatu ijayo, KM aliyahimiza Mataifa Wanachama kujitahidi kuiheshimu kidhati siku hiyo kwa kujitayarisha tangu sasa hivi ili kuhakikisha wakati utakapowadia wa kuiadhimisha siku hiyo vurugu na mabavu yatakomeshwa, na uhasama na mapigano yatasitishwa pote ulimwenguni.

Duru ya karibuni ya mikutano inayodhaminiwa na UM, kuzingatia udhibiti bora wa taathira za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, imehitmisha mijadala ya wiki mbili leo katika mji wa Bonn, Ujerumani. Mkutano ulijumuisha washiriki 2,000 kutoka nchi 170, na ilikuwa miongoni mwa mfululizo wa vikao vilivyoandaliwa kuendeleza mapatano ya UM kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa yanayotarajiwa kufikiwa 2009 kwenye mkusanyiko wa Copenhagen, Denmark.