OCHA yaomba dola milioni 150 kuhudumia kihali mamia elfu Kenya
Elizabeth Byrs, msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) amenakiliwa akisema kwamba kunahitajika haraka msaada wa dola milioni 150 kutoka wahisani wa kimataifa, ili kuhudumia kihali mamia elfu ya raia Kenya waliodhurika kihali kutokana na machafuko ya kisiasa yaliofumka nchini mwao kufuatia uchaguzi wa mwisho wa 2007.