Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECA yaanzisha vikao vya kuharakisha huduma za maendeleo Afrika

ECA yaanzisha vikao vya kuharakisha huduma za maendeleo Afrika

Abdoulie Janneh, Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo ya Uchumi Afrika (ECA) Alkhamisi alianzisha rasmi, kwenye Makao Makuu ya ECA yaliopo Addis Ababa, kikao cha mikutano ya kuzingatia suluhu ya kuridhisha kwa matatizo ya huduma za maendeleo Afrika. Warsha huu utakuwa unafanyika kila baada ya miezi sita, na hujumuisha wahisani wa kimataifa, wadau muhimu wanaojihusisha na maendeleo ya kiuchumi na jamii barani humo pamoja na wataalamu wa kutoka Baraza la ECA. ~