Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ongezeko la harakati za kijeshi mipakani Ethiopia/Eritrea kutia wasiwasi jamii ya kimataifa

Ongezeko la harakati za kijeshi mipakani Ethiopia/Eritrea kutia wasiwasi jamii ya kimataifa

Ripoti ya karibuni ya KM wa UM kuhusu hali mipakani kati ya Ethiopia na Eritrea, yaani kwenye ile sehemu ya Pembe ya Afrika ijulikanayo kama Eneo la Usalama wa Muda (TSZ), imeonekana kuwa ni ya wasiwasi mkubwa.

Ripoti ilisema Eritrea imepeleka silaha nzito za vita na wanajeshi 2,500 kwenye Eneo hilo la TSZ, na wakati huo huo mataifa yote mawili yameonekana yakiendeleza mazoezi ya kijeshi mipakani. Kadhalika ripoti imesema vikwazo dhidi ya helikopta za UM, ikijumuika na vizuizi dhidi ya kazi za wahudumia amani wa UM bado havijaondoshwa na Eritrea na vinaendelea kuzorotisha ulinzi wa amani. KM amenasihi nchi zote mbili kuruhusu ile Kamisheni ya Kuweka Mipaka kuendeleza kazi zake bila vizingiti ili kurudisha tena utulivu na amani mipakani.