Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yahudumia uboreshaji wa afya ya mama Tanzania

UNFPA yahudumia uboreshaji wa afya ya mama Tanzania

Karibuni UM ilichanganyika na Serikali za Mataifa Wanachama pamoja na mashirika ya kiraia kadhaa kuanzisha kampeni ya kimataifa, yenye lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito katika mataifa yanayoendelea, ikiwa miongoni mwa majukumu ya kutekeleza Malengo ya MDGs kwa wakati.

UNFPA ni shirika ambalo linashughulika na idadi ya watu. Yaani hili ni shirika ambalo ninafikiri linafahamu kwamba labda Tanzania kuna watu wangapi. Watoto wangapiwamezaliwa … Mimi kwa upande wangu nafikiri mchango wao ni mkubwa. Tena ni mkubwa sana tu, kwa sababu kwa muda mfupi ambao nimeweza kufika hata kwenye ofisi za UNFPA, nimeweza kuona ni jinsi gani wanashirikiana. Unaona kabisa taarifa zinafika, taarifa zinarudi na watu wanajumuika kwa pamoja kuweza kuyatekeleza masuala mazima ya kusaidia jamii

Stara alipendekeza maoni fulani ambayo angelipenedelea kuona yanatekelezwa haraka ili kuamsha zaidi hisia za umma juu ya umuhimu wa kudhibiti vyema uzazi na kupunguza vifo vya watoto wachanga:

Inabidi viwepo vipindi vya nyongeza vinavyoonesha ni jinsi gani mama anaanza process nzima ya uchungu, mpakakujifungua. Kuna vipengele fulani ambavyo vinasema mila na desturi na utamaduni; sasa tukiendekeza wakati mwingine hivi vitu bila kuvionesha wazi watu wakaelewa, mimi nafikiri tutakuwa tunapiga mark time somehow. Kwa sababu wakiweza kuona, angalau, itabadilisha baadhi ya watu. Halafu mbali la hilo, napenda kusema kwamba wanawake wote wa Tanzania na Afrika, na dunia, kwa ujumla, wafike katika vituo vya afya, mara tu wanapogundua wao ni wajawazito. Na wajitahidi kadri ya uwezo wao, wazalie katika vituo vya afya. Kwa sababu kufanya hivyo, kama tatizo linakuwepo, basi ni rahisi kutatuliwa, na ndio maana unakuta hata wakianzia nyumbani, wanapopata tatizo wanakimbilia kule kule hospitali ambapo ndipo walikuwa wanatakiwa wafike mwanzo na wakina baba; mama anapofikia katika hatua ile au tatizo lolote linpojitokeza wakati yeye ni mja mzito, hakuna suala lengine lolote la kuzungumza zaidi ya kumwahisha mama mja mzito hospitali.