Mikutano ya daraja ya juu inazingatia amani ya Afghanistan na Iraq

23 Septemba 2007

Ijumamosi, wasikilizaji kulifanyika kikao cha hadhi ya juu hapa Makao Makuu kuhusu Iraq, kilichoongozwa na KM wa UM Ban Ki-moon na Raisi wa Iraq Nouri Al-Maliki.

Ijumapili, Septemba 23, KM Ban Ki-moon na Raisi Hamid Karzai wa Afghanistan waliongoza mkutano mwengine wa viongozi wa ngazi za juu kwenye Makao Makuu, kikao ambacho kilijumuisha mataifa na mashirika yalio wanachama wa Bodi la Ushauri na Ufuatiliaji wa Mpango wa Maendeleo ya miaka mitano katika Afghanistan, mradi ulioanzishwa Januari 2006 na Serekali ya Afghanistan pamoja na wahisani wa kimataifa. Wiki hii kikao kilitathminia maendeleo katika nchi na kukadiria misaada itakayohitajika kurudisha tena utulivu wa jamii, hali ya usalama na ufufuaji wa huduma za uchumi maendeleo nchini Afghanistan.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter