Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Walinzi wa Amani Duniani

Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Walinzi wa Amani Duniani

Tangu miaka mitano iliopita, UM uliweka kando tarehe 29 Mei kuwa ni siku ya kuadhimishwa rasmi mchango wa wafanyakazi wa kimataifa, waume na wake, wa kutoka kanda mbalimbali za dunia ambao walitumia ujuzi wao, chini ya bendera ya UM, kulinda na kuimarisha amani ya kimataifa, na kuwapunguzia mateso ya hali duni umma wa kimataifa, pamoja na kuendeleza haki za binadamu na kudumisha huduma za maendeleo katika sehemu kadha wa kadha za ulimwengu.

Kama inavyoeleweka idadi za operesheni za amani za UM katika miaka ya karibuni zimekithiri na kuvunja rikodi.

Tumekuandalieni ripoti inayowakilisha sauti za baadhi ya walinzi wa amani wa UM kutoka Afrika Mashariki, wanaotumikia Shirika la UNMEE liliopo mipakani Ethiopia na Eritrea. Stella Vuzo, mtayarishaji vipindi vya Radio UNMEE alihojiana nao.

Kwa maelezo kamili sikiliza idhaa ya mtandao.