Skip to main content

Ripoti juu ya juhudi za karibuni kupiga vita malaria

Ripoti juu ya juhudi za karibuni kupiga vita malaria

Hivi karibuni takwimu za UM zilithibitisha ya kuwa watu milioni 300 hadi 500 huambukizwa maradhi ya malaria duniani, kila mwaka, na kati ya idadi hiyo watu milioni 1 hufariki, asilimia kubwa yao ikiwa watoto wachanga kutoka bara la Afrika.

Marie-Paule Kieny, Mkurugenzi katika Shirika la UM juu ya Afya Duniani (WHO) anayehusika na Mradi wa Utafiti wa Tiba ya Malaria alishiriki karibuni kwenye warsha maalumu wa siku nne mjini Bangkok, Thailand uliozingatia dawa ya chanjo. Kwenye risala yake alibashiria pindi jumuiya ya kimataifa itafanikiwa kuvumbua dawa ya chanjo kinga dhidi ya malaria, itakayosidia kukomesha malaria kwenye maeneo yanayosumbuliwa sana na ugonjwa huo, hasa barani Afrika, kitendo hicho kitawasilisha mafanikio makubwa kabisa ya kihistoria kuambatana na afya ya jamii.