Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ninaona nilichelewa kutambua umuhimu wa mazingira, sitaki itokee hivyo kwa wengine- Anita Soina

Ninaona nilichelewa kutambua umuhimu wa mazingira, sitaki itokee hivyo kwa wengine- Anita Soina

Pakua

Anita Soina wa nchini Kenya, msichana mwenye umri wa miaka 20 anasema anajiona ni kama alichelewa sana kujiunga katika harakati za kuyatetea mazingira ya ulimwengu. Anita Soina anaona kuna umuhimu mkubwa watoto kufahamu mapema katika umri mdogo kuhusu umuhimu wa mazingira bora ya ulimwengu na namna uharibifu wa mazingira unavyoweza kuhatarisha mstakabali wao. Kutokana na mtazamo huo, sasa Anita Soina yuko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa vijana na hata watoto wamefunzwa umuhimu wa kutunza mazingira. Akiwa yeye ni muasisi na Mkurugenzi wa shirika la Spice Warriors, Anita pia ameandika kitabu kinachofunza kuhusu mazingira kwa jina  Green War. Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amemhoji  Anita kuhusu harakati zake za kutunza mazingira
 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi/Anita Soina
Audio Duration
3'34"
Photo Credit
World Bank/Sue Pleming