Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ninatumia nishati ya jua katika ufugaji wa samaki - George Muga

Ninatumia nishati ya jua katika ufugaji wa samaki - George Muga

Pakua

Moja ya masuala yaliyojadiliwa kandoni mwa Mkutano wa ngazi ya juu ya siasa kuhusu maendeleo endelevu unaoendelea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, ni pamoja na namna waafrika wengi wanavyopambana na njia za zamani za nishati na hivyo kutafuta njia mbadala kama vile matumizi ya nishati ya jua. 

Mfano halisi ni huko nchini Kenya ambako mfugaji wa Samaki amepata mafanikio makubwa baada kuwekeza  kwenye vifaa vya nishati ya jua. George Muga anaelezea manufaa yaliyotokana na hatua aliyoichukua na pia kuwashauri wale walio na miradi inayotumia umeme.

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'21"
Photo Credit
UN Kenya/Neil Thomas