Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Ikiwa ni sehemu ya mradi wa 'kijani' wa UNDP, mafundi wakiweka mitambo ya nishati ya jua katika chuo cha polisi mjini Rajaf, Sudan Kusini 21 Agosti 2018

Ahadi ni deni: Mkutano wa kihistoria kutoa msukumo wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo.

UNDP/Louis Fourmentin
Ikiwa ni sehemu ya mradi wa 'kijani' wa UNDP, mafundi wakiweka mitambo ya nishati ya jua katika chuo cha polisi mjini Rajaf, Sudan Kusini 21 Agosti 2018

Ahadi ni deni: Mkutano wa kihistoria kutoa msukumo wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo.

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Umoja wa Mataifa unasema uchumi endelevu wa dunia ule ambao unailinda dunia  na kuboresha maisha ya kila mtu kila mahali ni fursa nzuri ya kuleta ajira na masoko yenye thamani ya matrilioni ya  dola. Ili kutimiza hilo , jamii ya kimataifa inahitaji kuongeza kasi ya uwekezaji.

Kwa azma ya kushawishi mataifa kuwekeza zaidi fedha kwenye maeneo ambayo yanaunga mkono Malengo 17  ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Umoja wa Mataifa unawaleta pamoja viongozi wa serikali, sekta ya biashara na makampuni ya kifedha jijini New York kesho Alhamisi, kushiriki kwenye mjadala mkuu wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufadhili kwa ajili ya maendeleo tangu kupitishwa kwa ajenda ya kuchukua hatua ya Addis Ababa mwaka 2015, ambayo iliweka safu ya hatua madhubuti  ili kubadilisha mazoea ya matumizi ya fedha duniani na kuelekeza uwekezaji wa fedha hizo katika kushughulikia changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa ikiwemo za kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kufanikiwa katika maendeleo endelevu kunaweza kuzalisha fedha zenye thamani ya dola trilioni 12 katika uchumi wa dunia, na kuleta ajira mpya milioni 380 ifikapo 2030.

Lakini kufikia azma hii kutahitaji uwekezaji wa dola trilioni 55 kila mwaka, katika sekta zote, kwa sasa viwango vya uwekezaji vinashuka sana chini ya kiwango hicho.

Sababu kadhaa zimetolewa kuelezea upungufu huu, kama vile ukuaji wa uchumi usio sawia, pengo la usawa, sababu zingine ni hatua zilizowekwa ambazo ni kiwazo cha biashara , kuongezeka kwa viwango vya madeni, na pengo la uwekezaji wa moja kwa moja toka nje ambavyp vimekuwa kizuizi kwauwezo wa  mataifa mengi kuwekeza katika utekelezaji wa maendeleo endelevu.

Msaidizi wa Katibu Mkuu kwa masuala ya kichumi na kijamii, Liu Zhenmin, ameambia UN News, “tukizingatia mabadiliko yanayohitajika, na mahitaji makubwa ya ufadhili, rasilimali binafsi zitalazimika kusaidia fedha za umma ambazo zinawakilisha uti wa mgongo wa rasilimali iliyopo. Kwa kuzingatia changamoto kubwa tunazokabiliana nazo, mabadiliko endelevu katika mifumo ya kifedha hayafanyiki kwa kiwango kinachohitajika, na kwa kasi inayotakiwa. Sekta ya fedha inazidi kuangaza hatari zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi na kuziweka katika michakato ya maamuzi ya uwekezaji. Pamoja na hayo, zana za kidijitali na uvumbuzi wa kifedha zinafungua vyanzo vipya vya fedha kwa maendeleo endelevu”.

Miradi inayoendelea barani Afrika

Barani Afrika, miradi inayoungwa mkono na Benki ya Dunia inaonyesha athari nzuri ambazo zinaweza kuletwa na maendeleo endelevu katika jamii. Jumuiya ya visiwa vya São Tomé na Príncipe, ambayo ina hatari ya kuathirika na mafuriko, mmomonyoko wa udongo na majanga ya asili, inanufaika na Programu ya Usimamizi wa Maeneo ya Pwani ya Afrika Magharibi, ambayo inasaidia serikali kuhusisha hatari za mabadiliko ya tabianchi inapopanga miundombinu kama vile barabara na majengo ya umma, na kuhakikisha kwamba vinajengwa mbali na pwani.

Moroco, ni moja wapo ya nchi zilizo mstari wa mbele katika harakati za mabadiliko ya tabianchi, inakabiliwa na mmomonyoko mkubwa wa udongo sehemu za  pwani, kuongezeka kwa joto, na kupungua kwa mvua. Miradi inayoungwa mkono na Benki ya Dunia imeisaidia serikali ya Moroco kukabiliana na athari za sera za mabadiliko ya tabianchi katika sekta tofauti za kiuchumi, na kumekuwa na  utumiaji mkubwa wa  nishati mbadala na kuboresha ufanisi wa nishati.

“Kufikia ya maendeleo endelevu kunahitaji mtazamo unaozingatia siku za usoni. Motisha za sekta za umma na za binafsi zinahitaji kwenda sanjari na maendeleo endelevu, ili maamuzi yote ya ufadhili wa kifedha yajumuishe uendelevu kama ni kitovu cha hatari inayowakabili.”, amesema Bwana Zhenmin.

Inatarajiwa kwamba mkutano huo utatumika kama wito wa hatua za pamoja za kuchochea nchi Wanachama na sekta binafsi kutangaza hatua mpya na halisi ambazo zitaongeza ufadhili kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kuhusu hatua dhidi ya fedha na ufadhili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa viwango vya fedha vya ufadhili wa muda mrefu wa mazingira yaktakayoruhusu  maendeleo endelevu ambayo yanatafuta kuchagiza afya na mustakabali wa watu na dunia.

Na pia wanahisa na wananchi kuchukua hatua za kudai kuwepo kwa uwekezaji unaojali mazingira , uwekezaji endelevu zaidi wa rasilimali, na matokeo yanayopimika , na ukweli endelevu ili kuongeza uwajibikaji na uwazi.