Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baadhi  ya vijana Tanzania bado wanashindwa kuhusisha SDGs na maisha yao- Hussein Melele

Baadhi  ya vijana Tanzania bado wanashindwa kuhusisha SDGs na maisha yao- Hussein Melele

Pakua

Vijana wengi nchini Tanzania wanaelewa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini si wengi wanaofahamu ni kwa namna gani malengo hayo yaliyopitishwa mwaka 2015 yanayahusiana moja kwa moja maisha yao. Hiyo ni kauli ya kijana Hussein Melele,  Mkurugenzi wa Mulika Tanzania, ambayo ni asasi ya kiraia inayowahamasisha vijana kushiriki katika masuala mablimbali ya kijamii. Mapema mwezi huu akihojiwa na Flora Nducha kandoni mwa jukwaa la ngazi ya juu la kutathimini SDGs mjini New York Marekani, Hussein alieleza namna ambavyo wanatumia taasisi yao inahaha kuhakikisha kwamba inatekeleza miradi ambayo kwayo inaweza kusaidia vijana kutambua uhusiano kati ya SDGs na maisha yao. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Flora Nducha/ Hussein Melele
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania