Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TAMWA yapigia chepuo mazingira salama shule ili hedhi isimkwamishe mtoto wa kike

TAMWA yapigia chepuo mazingira salama shule ili hedhi isimkwamishe mtoto wa kike

Pakua

Lengo namba 4 la malengoi ya maendeleo endelevu, SDGs linapigia chepuo suala la elimu kama chombo cha kumwezesha binadamu kujinasua kwenye umaskini na kuhimili mazingira  yake.

Hata hivyo lengo hhili linachambuliwa zaidi likitaka kila mwanafunzi awe wa kike au wa kiume awe katika mazingira bora ya kumwezesha kupata elimu hiyo bila kujali jinsia yake. Mathalani mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi,  isiwe kikwazo cha yeye kupata mafunzo na stadi kama wanazopata wanafunzi wa kiume.

Uzoefu unaonyesha kuwa ukosefu wa mazingira salama na safi shuleni husababisha watoto wa kike kushindwa kufika shuleni wakiwa kwenye hedhi. Suala hilo ni tatizo duniani na Tanzania nayo haijaepukika.

Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana chama cha wanahabari wanawake nchini humo,  TAMWA, kupitia ajenda yake ya kutetea haki za wanawake na watoto kwa njia ya vyombo vya habari, wameanzisha kampeni ya mazingira salama shuleni ili kuhakikisha hedhi si kikwazo kwa mtoto wa kike kupata elimu.

Je ni nini kinafanyika? Bi. Leonida Kanyuma, Afisa Miradi wa TAMWA anazungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na anaanza kwa kueleza wanaamaanisha nini wanaposema mazingira salama.

Audio Credit
Siraj Kalyango/ Anold Kayanda
Audio Duration
3'20"
Photo Credit
UNHCR/Catherine Wachiaya