Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoa bila vyeti Burundi si ndoa tena

Ndoa bila vyeti Burundi si ndoa tena

Pakua

Mwanamke wa Burundi akielimika anaweza kujitegemea na kufanya kila kitu kujikimu kimaisha ikiwemo kujua haki zake na kuzipigania. Amesema hayo afisa habari katika wizara ya mambo ya nje ya Burundi, Sonia Niyubahwe Ines, alipozungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii. Bi. Ines amesema hata hivyo kuna hatua kubwa zilizopigwa na serikali kuhakikisha mwanamke anakombolewa ikiwemo kutoa elimu bure kwa shule za msingi ili kumuhakikishia fursa ya kusoma mtoto wa Kike kama wa kiume lakini pia kupitisha sheria mbalimbali ikiwemo ya kila wanandoa kuwa na vyeti maalum, na kutenga asilimia 30 ya viti bungeni kwa ajili ya wanawake. Kwa undani zaidi ungana nao katika makala hii ambapo Ines anaanza kufafanua mafanikio yaliyofikiwa.

Soundcloud
Audio Credit
Anold Kayanda/Flora Nducha
Sauti
3'40"
Photo Credit
FAO/Giulio Napolitano