Ukosefu wa chakula bado changamoto Burundi
Pakua
Takwimu za mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi zinasema watu zaidi ya Milioni 3 nchini humo wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu. Watu milioni moja kati ya hao wana tatizo la ukosefu wa chakula. Hali hiyo imefanya watoto wengi kusumbuliwa na maradhi ya utapiamlo. Mashirika kadhaa ya wahisani yameanza kujishughulisha na kuwapa chakula watoto wenye tatizo la utapia mlo. Kufuatia hali hiyo , Burundi inajikuta katika wasiwasi mkubwa wa kuweza kutimiza lengo la maendeleo endelevu la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030 . Mwandishi wetu wa maziwa Makuu , Ramadhani KIBUGA ametembelea kituo kimoja kinachotoa chakula kwa watoto ili kupambana na njaa na utapia mlo.Ungana naye katika makala hii
Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango /Ramadhani Kibuga
Audio Duration
4'7"