Wakati ni sasa wa kumuinua mwanamke wa kijijini: Sudan Kusini
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yamefanyika juma hili kila kona ya dunia. Kauli mbiu ikiwa “Wakati ni sasa wa kumuinua na mkomboa mwanamke wa kijijini”
Huko Sudan Kusini maadhimisho yaliambatana na burudani ya ngoma za asili na ujumbe wa kudumisha amani na hasa ulinzi na usalama kwa kuwashirikisha zaidi wanawake ambao ni waathirika wakubwa wa machafuko.
Watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, wanaharakati wa haki za wanawake, na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia mkuu wa mpangu wa Umoja huo nchini Sudan Kusini David Shearer hakukosa. Basi ungana na Flora Nducha katika makala hii ujue mambo yalivyojiri