Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa vijana kuamka na kupiga kelele

Ni wakati wa vijana kuamka na kupiga kelele

Pakua

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kazi duniani, ILO  inaonyesha kuwa soko la ajira kwa vijana katika nchi zinazoendelea hususan katika bara la Afrika, Amerika kusini na Asia kusini linazidi kusuasua kutokana na ukuaji mdogo wa uchumi katika nchi hizo.

Umoja wa mataifa katika ajenda 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs , inazihimiza serikali,  mashirika na asasi za kiraia kuwekeza katika taaluma au miradi itakayowawezesha vijana kujikwamuwa na tatizo la ajira ifikapo mwaka2030.

Kando mwa jukwaa la vijana kwa mwaka huu wa 2018, Patrick Newman alipata  fursa ya kuzungumza na kijana Rahma Abdallah mwita, kutoka Tanzania ili kupata taswira ya hali ya ajira kwa vijana nchini Tanzania.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
2'54"
Photo Credit
Vijana Tanzania. Picha:UNFPA/Tanzania