Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SUDAN KUSINI

Sudan Kusini

Mwakilishi Maalum wa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom akivishwa kitamaduni wakati wa ziara yake ya kwanza huko Rumbek na Aweil.
UNMISS/Gregório Cunha

“Sisi ambao tunaishi Juba, mara nyingi tunatazama mambo tukiwa na fikra za Juba. Tunahitaji kuzuru kwenye majimbo na kuelewa mazingira ambmo wananchi wanaishi na ninawahakikishia kuwa nitakuwa nafika hapa mara kwa mara na kuendelea kuzungumza nanyi. Haya siyo mazungumzo ya kwanza na ya mwisho.”

Nicholas Haysom, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na Mkuu wa UNMISS

SUDAN KUSINI

Tarehe 9 julai 2011, Jamhuri ya Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka Sudan na kuwa taifa jipya kabisa duniani kuwa huru. Kuzaliwa kwa taifa hilo ilikuwa ni ukomo wa miaka 6 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo mwezi disemba mwaka 2019 uhasama kati ya rais wa Sudan Kusini na Makamu wake uliibua vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha janga kubwa la kibinadamu.

MWAKILISHI WA KATIBU MKUU WA UN SUDAN KUSINI

Tarehe 15 mwezi Januari mwaka 2021, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alimteua Nicholas Haysom wa Afrika Kusini kuwa Mwakilishi wake Maalum nchini Sudan Kusini na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS. Amechukua nafasi ya David Shearer wa Uingereza aliyemaliza muda wake.

HABARI ZA UN KUHUSU SUDAN KUSINI

Bofya hapa kupata habari za Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini

ULINZI WA AMANI SUDAN KUSINI

Kwa kupitisha azimio 1996 (2011) tarehe 8 julai 2011, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliridhia kuwa hali nchini Sudan Kusini bado inatishia usalama duniani na katika ukanda husika. Baraza la Usalama lilianzisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, (UNMISS) ili kuimarisha amani na usalama na kuweka mazingira muhimu ya maendeleo.