Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani

DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani

Pakua

Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. 

Mratibu wa masuala ya dharura wa WFP huko mashariki mwa DRC Bi. Cynthia Jones amesema  hapo awali walipata bahati ya kuanzisha mpango ambapo walikuwa wanaweza ama kuwapatia wakimbizi wa ndani chakula au kuwapatia fedha taslimu na hiyo iliwaruhusu kutoa aina thabiti zaidi ya usaidizi lakini kwa sasa hali ilivyo watalazimika kufanya maamuzi magumu. 

“Sasa hivi tulikuwa katika hali ambayo tunajitahidi kufikia watu milioni 1.2 na sasa tuna wakimbizi wengine milioni 1.2 wameongezeka. Na kwa hivyo itamaanisha tunapaswa kufanya maamuzi magumu juu ya jinsi tunavyotanguliza nani atakula na nani asile. Tunajaribu kuchukua rasilimali tulizo nazo na kuzitumia vyema na kuzisambaza, lakini sio jambo la maana kwani kitendo hicho ni kusema tuna sawazisha hali mbaya zaidi ya Kivu Kaskazini ni kwamba tunapaswa kupungua, inaweza kuwa ituri au Kivu Kusini. Hayo pia ni maamuzi magumu kwa sababu kuna watu wengi ambao hawana uhakika wa chakula katika maeneo hayo pia.”

Bi.Jones amesema pamoja na kuwa na fahari na kazi kubwa waliyoifanya ya kusaidia wakimbizi wengi hapo awali, mtiririko mkubwa wa wakimbizi wanaowasili kusaka hifadhi katika makambi katika miezi ya hivi karibuni umefanya kazi yao kuwa ngumu zaidi.

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
1'49"
Photo Credit
© WFP/Michael Castofas