Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 MACHI 2024

25 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akianzia na siku ya kimataifa ya kukumbuka watumishi wa UN wanaoshikiliwa vizuizini na wasiofahamika waliko, kisha anakwenda Sudan Kusini na harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono. Makala ni harakati za kumkomboa mwanamke na mashinani arejea Sudan Kusini.

  1. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu kuenzi ujasiri na kujitolea kwa wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kila mahali kokote waliko kwa kuahidi kuwalinda na kuwaunga mkono wanaposaidia kujenga dunia yenye amani zaidi na ya utu kwa ajili ya watu wote. Assumpta Massoi anaeleza zaidi.
  2. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
  3. Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya ambako mkutano wa maandalizi wa asasi za kiraia umekunja jamvi hivi karibuni na Stella Vuzo wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi alizungumza na Carole Osero-Ageng'o Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo. Anazungumzia harakati za kumkomboa mwanamke.
  4. Mashinani ni mlinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kutoka taifa la Bhutan.
Audio Credit
ANOLD KAYANDA
Audio Duration
11'42"